Je Muwasho ktk Ujauzito huwa ni Dalili ya nini? | Mambo gani ya kufanya ili kuondokana na muwasho?
Автор: Dr. Mwanyika
Загружено: 2021-03-07
Просмотров: 69544
Mambo yanayopelekea kupata Muwasho katika Ujauzito wako ni kama ya fuatayo;
Mimba inaweza kusababisha ukapata Muwasho kutokana na sababu kuu mbili;
1. Mabadiliko ya Homoni wakati Ujauzito.
2. Ongezeko la Tumbo wakati wa Ujauzito hususani kwenye Mimba ya kwanza au Mimba ya Mapacha.
Pamoja na hizo sababu lakini kuna Makundi makuu matatu yanayopelekea kupata Muwasho wa ngozi katika Ujauzito ambayo ni.
A. Kundi la kwanza ni Mtindo wa Maisha ya Mjamzito kama.
I. Kuvaa Nguo zinazobana ktk kipindi cha Ujauzito.
II. Kuvaa Nguo zisizo tengenezwa na Pamba.
III. Kuoga Maji ya Moto.
IV. Kutumia Sabuni na Perfume zinazo pelekea muwasho katika Ujauzito.
V.Ngozi ya Tumbo kukauka na kuvutika.
NB:Endapo una dalili tajwa hapo juu na unatabia hizo tajwa unachotakiwa kufanya ni kuchana na tabia hatarishi na pia unaweza kutumia MAFUTA YA NAZI AU CALAMINE LOTION.
B.Kundi la pili ni kuhusiana na Magonjwa ya Ngozi katka Ujauzito!
Mfano: Pruritic Urticaria Papules na Plaques vile Prurigo, hapa unahitaji kuonana na Daktari Bingwa wa Ngozi.
C. Endapo upo katika Kundi hili la tatu ni hatari sana unahitaji kuonana na Daktari bingwa na kutazamwa kwa Ujirani zaidi kwa sababu huweza kuathiri Afya ya Mtoto na Mama pia hii ni kutokana na shida iitwayo Intrahepatic Cholestasis of Pregnancy (ICP). Katika kundi hili Mama huwa na dalili zifuatazo.
Kuwashwa kwenye viganja vya Mikono au Miguuni.
Muwasho huwa zaidi kipindi cha jioni/usiku.
Kuwa na historia ya kuwa na dalili hizo katika baadhi ya ndugu katika ukoo husika.
Kupata Choo cheupe.
Kupata Mkojo mweusi na nk.
NB; Uonapo dalili hizo wahi hospital kuonana na Daktari.
Je muwasho ktk Ujauzito husababishwa na nini? Bonyeza link hii ili kujifunza zaidi • Je Muwasho ktk Ujauzito huwa ni Dalili ya ...
Mtoto huanza kucheza tumboni mwa Mama Mjamzito miezi mingapi??? Bonyeza link hii ili kujifunza zaidi
• Mtoto huanza kucheza tumboni mwa Mama Mjam...
Ufanye nini ili kuondokana na upungufu wa Damu katka kipindi cha Ujauzito??. Bonyeza link hapa.
• Ufanye nini ili uondokane na Upungufu wa D...
Je Mjamzito hujifungua wiki ya ngapi na wakati gani Uchungu huweza kuanza na salama zaidi?
Bonyeza link hii kusikiliza.
• Mama mjamzito anaweza kujifungua kuanzia w...
NB: Ukitaka kujifunza zaidi ni fuatilie YouTube kwa jina la Dr.Mwanyika au bonyeza link hapo 👇👇👇👇
/ drmwanyika
Ukiwa unamaswali unaweza kuuliza hapa chini (kwenye comments za youtube).
Subscribe,Comment and Share
JapideAfya_Services
Your Health is Our Health
Instagram as @JapideAfya_Services
Facebook page as @JapideAfya_Services
©Dr.Mwanyika.
#MamaAfya
#Muwasho
#DrMwanyika
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: