Популярное

Музыка Кино и Анимация Автомобили Животные Спорт Путешествия Игры Юмор

Интересные видео

2025 Сериалы Трейлеры Новости Как сделать Видеоуроки Diy своими руками

Топ запросов

смотреть а4 schoolboy runaway турецкий сериал смотреть мультфильмы эдисон
dTub
Скачать

SERIKALI YA AWAMU YA NANE YAENDELEA KUIMARISHA MJI MKONGWE KUPITIA USHIRIKIANO NA WADAU

Автор: ASAM Online TV

Загружено: 2025-12-29

Просмотров: 849

Описание:

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Awamu ya Nane, inayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, itaendelea kushirikiana kwa karibu na wadau wa maendeleo wakiwemo wa sekta binafsi, kwa lengo la kuyaimarisha maeneo ya kihistoria hususan Mji Mkongwe, ili kulinda, kuhifadhi na kutunza alama za urithi na utamaduni kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji, Mhe. Shabaan Ali Othman, wakati wa uzinduzi rasmi wa Hoteli ya FORT VIEW LUXURY AND ACCOMMODATION iliyojengwa katika eneo la Stone Town, Zanzibar, ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Katika hafla hiyo, Mhe. Waziri amesisitiza umuhimu wa kuwekeza katika mafunzo ya ujuzi kwa vijana ili waweze kushindana katika soko la ajira, kwa kushirikiana na taasisi za mafunzo pamoja na wadau wa maendeleo. Aidha, ametoa wito kwa vijana kujitokeza na kuzitumia fursa zilizopo kama njia ya kujijengea maisha bora kiuchumi.

Vilevile, amewahakikishia wawekezaji kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji ili kuongeza ajira kwa vijana, kukuza sekta binafsi na kuchangia utatuzi wa changamoto ya ajira, ambayo ni miongoni mwa changamoto kubwa kwa vijana duniani kote.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Dkt. Aboud Suleiman Jumbe, amesema uzinduzi wa hoteli hiyo ni mfano bora wa utekelezaji wa maono ya Rais Dkt. Mwinyi katika kuwakaribisha na kuwawezesha wana Diaspora kurejea nyumbani na kuwekeza katika miradi ya kimkakati ya kitaifa, hususan katika sekta ya utalii na urithi wa mambo ya kale.

Dkt. Aboud amefafanua kuwa hoteli hiyo ina vyumba sita vya mtindo wa apartments, ambapo kila apartment ina uwezo wa kuchukua wageni wanne hadi sita. Ameongeza kuwa mradi huo unatarajiwa kukamilika ukiwa na mkahawa (café), eneo la makaazi pamoja na galeria ya sanaa na makumbusho (gallery).

Ameeleza kuwa ukarabati wa awali wa mradi huo tayari umegharimu kiasi cha Dola za Kimarekani 800,000 sawa na Shilingi za Tanzania bilioni 2.5, ikiwa ni hatua muhimu katika kuimarisha utalii na uhifadhi wa urithi wa Mji Mkongwe.

#AwamuYaNane
#MjiMkongwe
#UwekezajiZanzibar
#UtaliiNaUrithi
#VijanaNaAjira
#MapinduziMatukufu

SERIKALI YA AWAMU YA NANE YAENDELEA KUIMARISHA MJI MKONGWE KUPITIA USHIRIKIANO NA WADAU

Поделиться в:

Доступные форматы для скачивания:

Скачать видео mp4

  • Информация по загрузке:

Скачать аудио mp3

Похожие видео

BARABARA NYENGINE PAMOJA NA DARAJA KUBWA LAFUNGULIWA, MAHONDA - PANGATUPU

BARABARA NYENGINE PAMOJA NA DARAJA KUBWA LAFUNGULIWA, MAHONDA - PANGATUPU

Inside The Burj Khalifa How the $1.5 Billion World's Tallest Building Was Built!

Inside The Burj Khalifa How the $1.5 Billion World's Tallest Building Was Built!

Zanzibar, eneo na mipaka yake kwa mtazamo wa kisheria na kihistoria-URITHI WETU (Episode 1):

Zanzibar, eneo na mipaka yake kwa mtazamo wa kisheria na kihistoria-URITHI WETU (Episode 1):

PAPO KWA PAPO! DKT. BASHIRU AKITATUA CHANGAMOTO ZA WANUFAIKA WA VIZIMBA VYA SAMAKI MARA!

PAPO KWA PAPO! DKT. BASHIRU AKITATUA CHANGAMOTO ZA WANUFAIKA WA VIZIMBA VYA SAMAKI MARA!

ZIARA YA KISAKASAKA

ZIARA YA KISAKASAKA

BAKHRESA AVUNJA REKODI ZANZIBAR

BAKHRESA AVUNJA REKODI ZANZIBAR

HUYU NDIE MFALME WAKWANZA ZANZIBAR.

HUYU NDIE MFALME WAKWANZA ZANZIBAR.

📺🔴: KWAHERI MOYALE VILIO NA DUA VYATANDA SHK KISHKI AKIAGWA.

📺🔴: KWAHERI MOYALE VILIO NA DUA VYATANDA SHK KISHKI AKIAGWA.

Orędzie noworoczne Prezydenta RP

Orędzie noworoczne Prezydenta RP

WAZIRI KITWANA KUKABIDHIWA RASMI TAWALA ZA MIKOA

WAZIRI KITWANA KUKABIDHIWA RASMI TAWALA ZA MIKOA

Sting - Every Breath You Take || Sylwester z Dwójką 2025

Sting - Every Breath You Take || Sylwester z Dwójką 2025

WAFANYAKAZI WADAI KUDHALILISHWA NA BOSS WAO RAIA WA UJERUMANI

WAFANYAKAZI WADAI KUDHALILISHWA NA BOSS WAO RAIA WA UJERUMANI

ZANROADS YATOA ONYO KALI KWA WANANCHI DHIDI YA KUTUMIA HIFADHI YA BARABARA

ZANROADS YATOA ONYO KALI KWA WANANCHI DHIDI YA KUTUMIA HIFADHI YA BARABARA

Zoezi Maalum la kuondosha Vibanda vya Barabarani

Zoezi Maalum la kuondosha Vibanda vya Barabarani

Putin Sends New Year Greetings, Voices Support for Troops in Ukraine Conflict

Putin Sends New Year Greetings, Voices Support for Troops in Ukraine Conflict

Hii Ndio Oman Watu Hawakuambii: Kazi, Mishahara Mikubwa na Usalama Usio wa Kawaida.

Hii Ndio Oman Watu Hawakuambii: Kazi, Mishahara Mikubwa na Usalama Usio wa Kawaida.

WAZIRI NADIR ATOA ONYO KALI KWA WACHIMBAJI WA MCHANGA KASKAZINI UNGUJA

WAZIRI NADIR ATOA ONYO KALI KWA WACHIMBAJI WA MCHANGA KASKAZINI UNGUJA

Mkurugenzi Mkuu wa ZARTSA awaondosha wafanyabiashara waliopo pembezoni mwa barabara.

Mkurugenzi Mkuu wa ZARTSA awaondosha wafanyabiashara waliopo pembezoni mwa barabara.

SOKO JIPYA LA KWEREKWE ZANZIBAR

SOKO JIPYA LA KWEREKWE ZANZIBAR

Maandamano yaenea Iran kwa siku ya 3 baada ya sarafu kufikia kiwango cha chini kuwahi kutokea

Maandamano yaenea Iran kwa siku ya 3 baada ya sarafu kufikia kiwango cha chini kuwahi kutokea

© 2025 dtub. Все права защищены.

  • Контакты
  • О нас
  • Политика конфиденциальности

Контакты для правообладателей: [email protected]