ZANROADS YATOA ONYO KALI KWA WANANCHI DHIDI YA KUTUMIA HIFADHI YA BARABARA
Автор: ASAM Online TV
Загружено: 2025-12-29
Просмотров: 1564
Wakala wa Barabara Zanzibar (ZANROADS) imewataka wananchi wote kuacha mara moja kutumia maeneo ya hifadhi ya barabara kwa shughuli zisizo rasmi ikiwemo ujenzi holela, biashara pamoja na kuegesha au kulaza magari pembezoni mwa barabara.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Wakala wa Barabara Zanzibar (ZANROADS), Ndugu Cosmas Masolwa, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za wakala huo, Saateni, Wilaya ya Mjini Zanzibar.
Amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya wananchi kutumia hifadhi ya barabara kwa matumizi mengine yasiyoruhusiwa kisheria, hali inayochangia kuharibu miundombinu ya barabara na kuhatarisha usalama wa watumiaji wa barabara. Amesisitiza kuwa ZANROADS haitasita kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mtu yeyote atakayekiuka agizo hilo.
Ndugu Masolwa amefahamisha kuwa Wakala wa Barabara Zanzibar ni taasisi ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, yenye jukumu la kusimamia, kudhibiti na kuhakikisha matumizi sahihi ya barabara kwa maslahi ya wananchi na maendeleo ya Taifa.
Mwisho, ZANROADS imewataka wananchi kushirikiana na serikali kwa kutunza miundombinu ya barabara na kuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa, ili kulinda usalama na kuendeleza maendeleo ya Zanzibar.
#ZANROADS
#HifadhiYaBarabara
#UsalamaBarabarani
#Zanzibar
#BreakingNews
#HabariMpya
#TrendingTikTok
#TrendingYouTube
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: