JESHI LA POLISI ZANZIBAR LATOA ONYO KALI KWA TIMU VIJROA, KADHAA WAWEKWA MBARONI
Автор: ASAM Online TV
Загружено: 2026-01-01
Просмотров: 300
Jeshi la Polisi limewataka wananchi kuzingatia kikamilifu sheria za barabarani pamoja na kufuata kanuni za kitamaduni na maadili ya Kizanzibar, hususan katika matamasha, sherehe na maonyesho ya mavazi na tamaduni yanayofanyika katika maeneo ya kihistoria.
Tamko hilo limetolewa na Senior Assistant Commissioner wa Kituo cha Polisi Tunguu, Ndugu Josephy Danieli Shillah, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kufuatia kukamatwa kwa vijana waliokodi magari mawili aina ya roli, yaliyobeba idadi kubwa ya watu waliokiuka sheria za barabarani na maadili ya Mzanzibar huko Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema kuwa kukamatwa kwa magari hayo kumetokana na ushirikiano mkubwa kati ya Jeshi la Polisi, Baraza la Sanaa Zanzibar pamoja na Mamlaka ya Usafiri Zanzibar, ambapo magari mawili yenye namba Z 667 GZ na Z 692 AAD yalikamatwa yakibeba vijana waliokuwa wakipiga muziki unaokiuka maadili na kuchafua taswira ya tamaduni za Kizanzibar.
Aidha, amesisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wahusika wote waliokiuka sheria hizo, ikiwemo kukosa vibali halali kutoka Jeshi la Polisi na Baraza la Sanaa Zanzibar, ili iwe fundisho kwa vijana wengine na kulinda heshima, maadili na utamaduni wa Zanzibar.
#Zanzibar
#PolisiZanzibar
#MaadiliYaKizanzibar
#SheriaZaBarabarani
#UtamaduniZanzibar
#AmaniNaUmoja
#TrendingTikTok
#TrendingYouTube
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: