ASKOFU SHOO: “KUMCHA BWANA NDICHO CHANZO CHA HEKIMA”
Автор: UMOJA DAIMA MEDIA
Загружено: 2025-11-21
Просмотров: 372
Mkuu wa Kanisa la Kiinjjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini, Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo amesema kuwa kumcha Bwana ndiyo msingi wa hekima, akisisitiza kuwa maisha ya Mch. Dkt. Joshua Laizer ni ushahidi wa ahadi za Mungu kwa wanaomcha.
Akizungumza katika Ibada ya Shukrani Usharika wa Karansi Jimbo la Siha Novemba 21,2025, Askofu Shoo alimpongeza Dkt. Laizer kwa kutunukiwa Udaktari wa Heshima (PhD) kutoka Corner Stone and International Bible University.
Askofu Shoo amemkumbuka Dkt. Laizer alivyowasili Chuo cha Biblia na Theologia Mwika miaka iliyopita akiwa na shauku ya kumjua Mungu, akisema uwezo wake wa kujifunza ulionekana mapema:
“Kumcha Bwana ni chanzo cha hekima,” amesisitiza.
Akinukuu Yeremia 33:3: “Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua” amesema safari ya Dkt. Laizer imethibitisha neno hilo.
Amesema Mch. Laizer ametumia vipawa vyake kwa bidii kwenye jamii, hasa katika kabila la Kimaasai, ambako ameeneza Injili, kusuluhisha migogoro, kuelimisha na hata kuandika historia ya jamii hiyo.
“Mcha Mungu hupata si maarifa tu, bali hekima, nguvu na uwezo,” amesema, akimtakia Dkt. Laizer kutumia heshima hiyo kulitumikia Kanisa kwa bidii zaidi.
Askofu Shoo amewatia moyo wachungaji na wainjilisti kuendelea na kazi ya Bwana kwa uaminifu na msukumo wa ndani.
Kabla ya kuaanza kwa ibada hiyo Askofu Dkt. Shoo aliweka jiwe la msingi jengo la Kanisa Mtaa wa Sabuko, Nyumba ya Ibada ya watoto wa shule ya Jumapili Mtaa wa Kandashi na Bwalo la kituo cha watoto wenye uhitaji maalum Usharika wa Karansi. Pia alifungua ofisi ya Mtaa wa Neema na ofisi ya Senta ya Usharika wa Karansi.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: