ASKOFU JOHN MAGUGE ATOA WITO MAANDALIZI YA HUKUMU YA MWISHO KATIKA UFUNGUZI WA NYUMBA YA IBADA KYUU
Автор: UMOJA DAIMA MEDIA
Загружено: 2025-11-16
Просмотров: 871
Askofu John Maguge wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mkoani Mara ametoa mahubiri yenye kufundisha kuhusu umuhimu wa waumini kujiandaa kwa Hukumu ya Mwisho, akisisitiza kuwa hukumu ya Mungu si jambo jepesi na si sawa na hukumu za kibinadamu tunazozizoea hapa duniani.
Akihubiri katika ibada ya ufunguzi wa nyumba ya ibada ya Usharika wa Kyuu, Jimbo la Hai, Askofu Maguge amesema waumini wanapaswa kuishi maisha ya kutubu na kusema ukweli mbele za Mungu, kwa kuwa tofauti na duniani, ambapo anakiri kosa kunamweka mtu hatarini, mbele za Mungu toba humletea msamaha.
Ibada hiyo imeongozwa na Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini, Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo, akishirikiana na Msaidizi wake Mch. Deogratius Msanya, Mkuu wa Jimbo la Hai Mch. Biniel Malyo, pamoja na Mch. Emilly Peter Haishi, mchungaji kiongozi wa Usharika wa Kyuu.
Katika mafundisho yake, Askofu Maguge amesisitiza kuwa Mungu hutazama ukweli wa moyo wa mtu, na kwamba hukumu ya Mungu si ya muda bali ni ya milele. Ameonya kwamba baadhi ya waumini hudhani uwepo wao kanisani unawapa haki, ilhali ndani yao bado hawajafanya toba ya kweli.
Akinukuu mifano ya biblia kama wa Anania na Safira, Askofu Maguge alionya dhidi ya udanganyifu na majivuno, akisema mfano huo unaonyesha jinsi Mungu anavyochukia uongo na mioyo isiyo na toba.
Aidha, akifananisha hukumu ya mwisho na mvuvi anayeuchambua wavu baada ya kuvua, Askofu Maguge alisema siku ya mwisho Mungu atawatenganisha wenye haki na waovu kama samaki wazuri na wabaya.
Amehimiza waumini kutubu kila mara na kuishi maisha ya kumpendeza Mungu.
“Mungu hana shida na dhambi zako, shida yake ni kutokutubu kwetu,” amesisitiza.
Askofu Maguge amewakumbusha waamini kuwa hawajui siku wala saa ya kuja kwa Bwana, hivyo wahakikishe wanaishi Maisha ya toba ya kudumu, pasipo uoga wala kiburi cha kiroho.
Amewahimiza kushika Neno la Mungu na kulitendea kazi, akiwataka waumini kutumia nafasi wanayopewa sasa kwa ajili ya kutubu ili siku ya hukumu wapate kusamehewa.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: