NENO LA SIKU | Mathayo 21 | Maombi Ya Kuvunja Laana | Isaac Javan
Автор: Neno La Siku
Загружено: 2024-03-05
Просмотров: 10433
Leo tunasoma kitabu cha Mathayo sura ya ishirini na moja. Na siku ya leo tunaenda kufanya maombi ya kuvunja laana. Vifungo vya laana ni moja ya vifungo vinavyotesa maisha ya watu wengi.
Kuna kifungo cha laana kinachofanya kazi kwenye maisha ya mtu binafsi, lakini pia kuna kifungo cha laana kinachofanya kazi kwenye familia au ukoo. Na vyote vina madhara makubwa sana ya kiroho.
Katika somo la leo, utajifunza maana ya laana, na vyanzo vyake. Lakini pia utapata nafasi ya kuomba pamoja na mimi, ili kwa pamoja tuweze kuvuka na kuvishinda vifungo vya laana vinavyofuatilia maisha yetu.
Nakuombea YESU akukumbuke, na akufungue siku ya leo. Nakushauri utakapokuwa unaomba, omba kwa kumaanisha ili uweze kupata matokeo mazuri ya maombi haya. Mungu akubariki sana na kukutunza. Amen
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: