TAZAMA UZURI WA MJI WA SINGIDA ,ZIWA KINDAI NA SINGIDANI .
Автор: MLIMBA TV
Загружено: 2024-07-07
Просмотров: 562
Mkoa wa Singida upo katikati ya Tanzania Bara. Mji wake Mkuu ni Singida na ni njia panda muhimu kwa usafiri wa barabara kwenda Kaskazini, Magharibi, Kusini na Mashariki.
Singida inapakana na Mkoa wa Manyara kwa upande wa Kaskazini, Mkoa wa Dodoma upande wa Mashariki, Mikoa ya Mbeya na Iringa upande wa Kusini na Mikoa ya Tabora na Simiyu upande wa Magharibi.
Mkoa wa Singida ulianzishwa rasmi tarehe 15 Oktoba, 1963 ambapo kabla ya hapo ulikuwa ni Wilaya ya Jimbo la Kati (Central Province) uliojumuisha Mkoa wa Dodoma.
Mkoa wa Singida uko katikati ya Tanzania, kati ya Longitudo 33027’5’’ na 35026’0’’ mashariki ya Greenwich, na kati ya latitudo 3052’ na 7034’ Kusini mwa Ikweta.
Mkoani Singida ndipo kuna eneo eneo rasmi ambalo lilibainishwa na vipimo vya kitaalamu vyenye namba 9305404.35, 698978.015 kuwa ni katikati mwa Tanzania bara yaani Central point of Tanganyika, ambapo ni katika kitongoji cha Darajani, Kijiji cha Chisingisa kilichopo kata ya Sasilo, tarafa ya Nkonk’o Wilaya ya Manyoni.
Mkoa wa Singida una Wilaya 5 ambazo ni Singida, Iramba, Manyoni, Mkalama na Ikungi; zenye Halmashauri 7 za Singida, Singida Manispaa, Iramba, Manyoni, Mkalama, Ikungi na Itigi. Aidha Mkoa una Tarafa 21, kata 136, Vijiji 442, vitongoji 2,309 na majimbo ya uchaguzi 8.
Ukubwa wa eneo la Mkoa wa Singida ni kilomita za mraba 49,341 sawa na asilimia 6 ya eneo la Tanzania Bara ambapo kati ya hizo kilomita za mraba 11,340 zinafaa kwa kilimo sawa na asilimia 23 ya eneo lote la Mkoa.
Kwa upande wa hali ya hewa Mkoa wa Singida hupata mvua kwa kipindi kimoja cha mwaka (mwezi Novemba hadi Aprili) kwa wastani wa milimita 500 – 800 kwa mwaka na wastani wa hali ya hewa ni nyuzi joto 15 – 30 kutegemea msimu na mwinuko wa ardhi. Kutokana na hali ya hewa, Mkoa wa Singida ni miongoni mwa Mikoa iliyopo kwenye ukanda wa unaopata mvua kidogo.
BAADHI YA MAENEO MUHIMU YA MJI WA SINGIDA ,KARIBU UFUATILIE CHANEL YAKO ,YA MLIMBA TV.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: