UFUNGUZI WA MAFUNZO KWA WASIMAMIZI NA WASIMAMIZI WASAIDIZI WA UCHAGUZI JIMBO LA MISSENYI
Автор: MISSENYIDC
Загружено: 2025-10-26
Просмотров: 201
Leo Oktoba 26, 2025 Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Missenyi Bi. Seraphina A. Rwegasira amefungua mafunzo ya siku mbili kwa Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo vya kupigia kura ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.
Akifungua mafunzo hayo katika Ukumbi wa KS Hotel uliopo Wilayani Missenyi, Bi. Seraphina amewataka Wasimamizi hao kutokuwa chanzo cha malalamiko kutoka kwa vyama vya siasa.
"Jitahidini na mjiepushe kuwa vyanzo vya malalamiko kutoka kwa vyama vya siasa kwa kuhakikisha mnashirikiana vyema na mawakala wa vyama vya siasa watakaokuwepo vituoni kwa mujibu wa Sheria", amesema Bi. Seraphina.
Aidha, amewataka Wasimamizi hao kufanya kazi kwa ushirikiano kama timu, ili kufanikisha Uchaguzi katika Vituo watakavyopangiwa.
Ikumbukwe kwamba Uteuzi wa Wasimamizi wa Vituo na Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo umezingatia masharti ya kifungu cha 76 (b) na (c) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, ambapo kifungu cha 76(b) kinasema "Msimamizi wa Uchaguzi atateua kwa kila eneo la uchaguzi idadi ya watu watakaojulikana kama wasimamizi wasaidizi wa vituo, kama atakavyoona inafaa kumsaidia msimamizi wa kituo wakati wa kupiga kura katika uchaguzi", na kifungu cha 76(c) kinaelekeza "Msimamizi wa Uchaguzi atateua kutoka miongoni mwa wasimamizi wasaidizi wa vituo mtu atakayekuwa kiongozi wa kituo ambaye atajulikana kama msimamizi wa kituo".
Mafunzo haya ya siku mbili yanahusisha Kata zote 20 za Wilaya ya Missenyi, yakiwa na lengo la kuwajengea ujuzi Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo kulekea siku ya kupiga kura Oktoba 29, 2025.
"Kura Yako Haki Yako Jitokeze Kupiga Kura"
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: