UFUNGUZI WA MAFUNZO KWA MAKARANI WAONGOZAJI WAPIGA KURA JIMBO LA MISSENYI
Автор: MISSENYIDC
Загружено: 2025-10-25
Просмотров: 152
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Missenyi Bi. Seraphina A. Rwegasira amefungua mafunzo kwa Makarani Waongozaji Wapiga Kura leo tarehe 25/10/2025.
Akifungua mafunzo hayo Bi. Seraphina amewasisitiza Makarani hao kuzingatia Sheria, kanuni na maelekezo watakayopewa hadi hapo Uchaguzi Mkuu utakapokamilika.
Mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika katika Jimbo la Missenyi, yakijumuisha Kata zote 20 ndani ya Wilaya ya Missenyi.
Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 unaongozwa na kauli mbiu isemayo: "Kura yako Haki yako Jitokeze Kupiga kura"
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: