SERIKALI YAANZA KUPANUA BARABARA KUU YA TANZAM ENEO LA MLIMA NYOKA ILI KUEPUSHA AJALI
Автор: BONGO PLAY TELEVISION
Загружено: 2026-01-17
Просмотров: 50
.
Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania, TANROADS, imeanza kupanua barabara kuu ya Tanzania na Zambia, TANZAM, katika eneo la mlima nyoka, nje kidogo ya jiji la mbeya kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari na ajali za mara kwa mara ambazo zimekuwa zikitokea katika eneo hilo na kusababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali za wananchi.
Meneja wa barabara kuu na barabara za mijini nchini, kutoka wakala wa barabara tanzania, tanroads, makao makuu, mhandisi nchama wambura ametasema hayo wakati alipotembelea eneo la mlima nyoka ambako kazi ya upanuzi wa barabara hiyo inaendelea….1. Eng. Nchama wambura – meneja wa barabara kuu na barabara za mijini kutoka taroads makao makuu.
Chifu wa kabila la wasafwa, ambao ni wenyeji wa eneo hilo, chifu Rocket Mwashinga akatoa baraka zake kwa serikali kutekeleza mradi huo katika eneo la asili la mlima nyoka.
Meneja Wa Tanroads Mkoa Wa Mbeya, Mhandisi Suleiman Bishanga akiwataka wataalam wanaotekeleza mradi huo kuwa waadilifu
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: