KIGAMBONI SASA KUPATA SHULE YA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM
Автор: Swahili Tv
Загружено: 2022-09-21
Просмотров: 664
#AfricaSwahuliWetePemaba#raissamia#FatmaNyagasa#
Bilioni 1.9 kutumika kwenye miradi 73 eneo la Elimu Msingi- DC Nyangasa
" Haya ni matokeo ya jitihada za Rais wetu Samia Suluhu Hassan katika kuboresha miundombinu ili kuhakikisha hakuna mtoto anayekosa haki ya msingi ya kupata elimu"
Ujenzi wa Shule ya kwanza Maalum kwaajili ya watoto wenye mahitaji Maalum uko katika hatua za kukamilika hali ambayo itaifanya Wilaya hii nayo kuwa na shule maalum kama ilivyo katika wilaya nyingine.
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Fatma Almas Nyangasa amesema hayo alipokuwa kwenye ziara maalum ya ukaguzi wa miradi katika sekta ya elimu ikiwemo ujenzi wa mabweni mawili kwaajili ya watoto wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi Chekeni Mwasonga.
DC Nyangasa amesema kiasi cha shilingi bilioni 1.937 zitatumika katika mwaka huu wa fedha kwaajili ya ujenzi , ukarabati na uendeshaji wa miradi 73 katika eneo la Elimu Msingi wilayani Kigamboni, ikiwa ni mjumuisho wa fedha zinazotoka serikali kuu, halmashauri na miradi inayofadhiliwa na wadau.
Jumla ya watoto 160 wenye mahitaji maalum wanatarajiwa kunufaika na mradi huu katika awamu hii ya kwanza.
"Tunamahukuru sana Rais wetu Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa serikali yake kuendelea kuelekeza fedha kuboresha miundombinu ya elimu kwaajili ya watoto wetu. Sasa na sisi (Kigamboni) tutakuwa na shule maalum ambapo watoto wetu wa kike na wa kiume wenye mahitaji maalum watakuwa na mazingira mazuri ya kupata elimu kulingana na mahitaji yao"
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: