KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA MORNING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 23/01/2026
Автор: KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH
Загружено: 2026-01-23
Просмотров: 5719
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA MORNING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 23/01/2026
UJUMBE WA LEO: MAMBO YA KUOMBEA KATIKA MSIMU MPYA
(Prayer Priorities for a New Season)
Mhubiri 3 : 1
Ni kukufahamisha maeneo muhimu ya kuombea katika msimu wako mpya ili uimarishe mahusiano yako na Mungu na ufanikiwe kimaisha.
5. KUPANGA NA KUOMBEA MIPANGO YAKO KATIKA MSIMU HUU MPYA
MAOMBI SI MBADALA WA MPANGO
Mafanikio ya kweli hayaji kwa bahati wala kwa msukumo wa hisia,
bali hujengwa juu ya kanuni sahihi na mifumo ya kiroho.
Mungu wetu ni Mungu wa mpangilio, si wa machafuko.
Hivyo basi, maombi hayakusudiwi kuchukua nafasi ya mipango,
bali kuyaimarisha na kuyaongoza.
Msimu mpya bila mpango ni sawa na safari bila ramani.
Utatumia nguvu nyingi njiani, lakini hutafika kwenye kusudi.
1 Wakorintho 14 : 33
33 Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu.
I. MAONO (VISION): KUONA KABLA YA KUTENDA.
Maono ni uwezo wa kuona hatima kabla ya safari kuanza.
Ni ufahamu wa kile Mungu alichokipandikiza ndani ya mtu
kwa ajili ya kizazi chake.
Yeremia 1 : 5
5 Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.
Maono huleta mwelekeo na nidhamu.
Bila maono, mtu huishi kwa kujibu matukio
badala ya kuyaongoza.
Mithali 29 : 18
18 Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.
II. MALENGO (GOALS): KUVUNJA MAONO KATIKA HATUA.
Maono ni picha kubwa ya maisha,
lakini malengo ni hatua za vitendo
zinazoifikisha picha hiyo katika uhalisia.
Maono bila malengo hubaki kuwa mawazo mazuri
yasiyo na matokeo yanayoonekana.
Mithali 4 : 26
26 Ulisawazishe pito la mguu wako, Na njia zako zote zithibitike;
Kupima kunampa mtu ufahamu wa mahali alipo
na mwelekeo wa mahali anapoelekea.
Malengo humjengea mtu nidhamu ya kukataa
mambo yasiyo ya lazima
ili kulinda kile kilicho cha msingi.
1 Wakorintho 9 : 25
25 Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika.
III. MIPANGO (PLANS): MFUMO UNAOLINDA MAONO
Mipango ni mifumo inayolinda maono yasije yakafa njiani.
Mungu hafanyi kazi kwa misukumo ya ghafla,
bali hufanya kazi kupitia mifumo iliyopangwa.
Mipango huonyesha kuwa unaiheshimu
rasilimali adhimu ya Ufalme (muda).
Mithali 21 : 5
5 Mawazo ya wenye bidii huuelekea utajiri tu; Bali kila mwenye pupa huuelekea uhitaji.
Mungu habariki bidii ya vurugu,
anabariki bidii iliyo chini ya mpango.
Mithali 20 : 18
18 Kila kusudi huthibitika kwa kushauriana; Na kwa shauri la akili fanya vita.
Msimu mpya bila mashauriano ni hatari.
IV. UTENDAJI (EXECUTION): LUGHA YA MAONO
Maono yasiyotekelezwa hubaki kuwa mzigo wa mawazo,
na mpango usiotendwa hubaki kuwa karatasi tu.
Utendaji ndiyo lugha ambayo maono
hujitambulisha duniani.
Yakobo 2 : 17
17 Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake.
Usisubiri hali iwe kamilifu ili uanze.
Anza na kile ulicho nacho, mahali ulipo,
na Mungu atakukabidhi zaidi.
Luka 16 : 10
10 Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia.
V. TATHMINI (EVALUATION): KIOO CHA UKOMAVU
Tathmini ni alama ya watu waliokomaa
kiroho na kiutawala.
Ni uwezo wa kujiuliza kwa uaminifu:
"Je, bado niko ndani ya mstari wa kusudi?”
Kanuni ya Ufalme ni hii:
Waliofanikiwa hujipima,
walioshindwa hujilaumu.
Maombolezo 3 : 40
40 Na tuchunguze njia zetu na kuzijaribu, Na kumrudia Bwana tena.
Tathmini hukurudisha kwenye mstari
kabla hujapotea mbali.
Mhubiri: Mwl. Davidney Kaale
Kwa maombi na ushauri :
Mch. Kiongozi: Dr. Eliona Kimaro
Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053
Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga
Simu: +255 713 553 443
YouTube: Kijitonyama Lutheran church
Barua Pepe : Kijitonyamalutheran@gmail.com
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: