MVUA YAACHA KILIO KAHAMA VILIO VIKITAWALA 'VINYESI VINAPITA PEDI'
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2025-01-08
Просмотров: 862
Mvua iliyonyesha wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga imeleta athari katika baadhi ya maeneo, ikijaza mitaro ya majitaka na kufurika katika makazi ya watu.
Wakizungumza na Mwananchi jana Januari 7, 2025, baadhi ya wananchi wa Kata ya Mulanga na Majengo wilaya ya Kahama wamesema maji hayo yamewakosesha makazi, kuharibu mali na kuhatarisha afya zao.
Akizungumzia kero hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita amesema, athari hizo zimesababishwa na uborashaji wa mji kupitia mradi wa uboreshaji miji (Tactics) katika Manispaa ya Kahama.
“Katika Kata za Mulanga na Majengo kumetokea athari hii kwa sababu kuna mradi wa uboreshaji miji katika wilaya yetu, ambapo pia kuna uchimbaji wa mitaro kwa ajili ya ujenzi wa barabara na hizi mvua zimekua zikinyesha kwa muda mrefu hasa nyakati za usiku.
“Tulichofanya ni kuhakikisha wakandarasi na Tarura (Wakala wa Barabara Mijini na Vijini) wako huko kurekebisha hilo na kuhakikisha na pia kasi a ujenzi inaongozeka ili kukamilisha haraka,” amesema Mhita.
Kaimu meneja wa Tarura Wilaya ya Kahama, Masola Juma amethibitisha kutokea kwa athari hizo kwa baadhi ya kata ambazo zimesababishwa na mvua zilizonyesha mfululizo na kuharibu barabara na kusababisha maji kwenda kwa wananchi.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: