Cheki vijana wa Mwanza walivyomiminika kuchangamkia ofa ya serikali
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2021-04-30
Просмотров: 1410
Mamia ya vijana wamemiminika katika chuo cha Veta kilichopo Nyakato jijini Mwanza ili kuomba nafasi ya kupatiwa mafunzo ya ufundi stadi kama yalivyotangazwa na serikali.
Serikali ilitangaza kufadhiri ada ya mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana 12,625 nchini ambapo mpaka jana mchana Aprili 30, Chuo cha Veta Mwanza kilikuwa kimepokea maombi ya vijana zaidi ya 1,800 wakiomba kupatiwa mafunzo hayo.
Akizungumza na Mwananchi, Revocatus Boniphace ameiomba serikali kuongeza idadi ya wadailiwa ili kutoa fursa vijana wasiyo na ajira kupatiwa mafunzo hayo.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: