SIKUKUU YA WATOTO | IBADA YA KWANZA | JUMAPILI | 28 / 09 / 2025
Автор: Azania Front Cathedral
Загружено: 2025-09-27
Просмотров: 871
Karibu katika Ibada ya Jumapili, siku ya 15 baada ya Utatu, kutoka hapa kanisa Kuu Azania Front Posta Dar Es Salaam.
SOMO: TUWAPENDE NA KUWAJALI WATOTO KATIKA BWANA
~ KUMBUKUMBU 6: 6 - 9
▶️MHUBIRI:
........................
🖋️ Masomo
~ ZABURI 113: 1 - 9
1 Haleluya. Enyi watumishi wa BWANA, sifuni, Lisifuni jina la BWANA.
2 Jina la BWANA lihimidiwe Tangu leo na hata milele.
3 Toka maawio ya jua hata machweo yake Jina la BWANA husifiwa.
4 BWANA ni mkuu juu ya mataifa yote, Na utukufu wake ni juu ya mbingu.
5 Ni nani aliye mfano wa BWANA, Mungu wetu aketiye juu;
6 Anyenyekeaye kutazama, Mbinguni na duniani?
7 Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Na kumpandisha maskini kutoka jaani.
8 Amketishe pamoja na wakuu, Pamoja na wakuu wa watu wake.
9 Huweka nyumbani mwanamke aliye tasa, Awe mama ya watoto mwenye furaha.
~ YOHANA 4: 46 - 54
46 Basi alifika tena Kana ya Galilaya, hapo alipoyafanya yale maji kuwa divai. Na palikuwa na diwani mmoja ambaye mwanawe hawezi huko Kapernaumu.
47 Huyo aliposikia ya kwamba Yesu amekuja kutoka Uyahudi mpaka Galilaya, alimwendea, akamsihi ashuke na kumponya mwanawe; kwa maana alikuwa kufani.
48 Basi Yesu akamwambia, Msipoona ishara na maajabu hamtaamini kabisa?
49 Yule diwani akamwambia, Bwana, ushuke asijakufa mtoto wangu.
50 Yesu akamwambia, Enenda; mwanao yu hai. Mtu yule akalisadiki lile neno aliloambiwa na Yesu, naye akashika njia.
51 Hata alipokuwa akishuka, watumwa wake walimlaki, wakisema ya kwamba mtoto wake yu hai.
52 Basi akawauliza habari ya saa alipoanza kuwa hajambo; nao wakamwambia, Jana, saa saba, homa ilimwacha.
53 Basi babaye akafahamu ya kuwa ni saa ile ile aliyoambiwa na Yesu, Mwanao yu hai. Akaamini yeye na wote wa nyumbani mwake.
54 Hiyo ni ishara ya pili aliyoifanya Yesu, alipokuwa ametoka Uyahudi kufika Galilaya.
...........................................................................................................................................
👇👇👇
KWA MAOMBI NA USHAURI :
☎️ +255 748 290 290
MCH. VICTOR MAKUNDI
// NAMBA ZA SADAKA //
▶ LIPA KWA [ M-PESA ] - 579 579 4
▶ NAMBA YA MPESA - 0757 - 391 - 174
JINA: KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
▶ MAENDELEO BANK
A/C NO 0137 9274 6021
JINA: LUTHERAN CHURCH AZANIA FRONT CATHEDRAL
TUFUATILIE KWENYE MITANDAO KWA TAHARIFA ZAIDI:
Instagram page:
/ kkkt_azaniafront_cathedral
Website: https://www.azaniafront.org/
Facebook:
/ kkkt-azania-front-cathedral-101434162039079
#azaniafrontcathedral #lunchhour #lutheran
........................
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: