RC KATAVI ASHIKA CHEPE NA KUJENGA SHULE| WATOTO WASOME| UCHAGUZI WA AMANI| BARABARA YA LAMI KAREMA.
Автор: HALMASHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA
Загружено: 2025-10-02
Просмотров: 122
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe Mwanamvua Hoza Mrindoko amevitaka wataalamu na wananchi kwa ujumla kuzingatia taratibu za kiusalama wakati wa utafutaji wa riziki ili kuepukana na madhara makubwa ambayo yanweza kuepukika kwa kuzingatia taratibu.
Mhe Mrindoko ameyasema hayo hii wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika Wilaya ya Tanganyika, ambapo ametembelea mradi wa ujenzi wa shule ya msingi iliyopo Sibwesa, amekagua ujenzi wa Barabara ya kiwango cha lami ya Kagwira- Kasekese na Kasekese- Karema na kuagiza ifikapo Desemba 31 mwaka huu kipande cha Kasekese- Karema kiwe kimeshakamilika.
Pia ametembelea Bandari ya Karema kujionea hatua iliyofikia ujenzi wa meli 4 za mizigo ambapo ameridhishwa na ujenzi huo.
“Niendelee kuagiza kanuni, taratibu, sheria pamoja na mikakati ya kiusalama izingatiwe zaidi wakati wa kufanya shughuli za kiuchumi, ili kuepuka kupata madhara au ajali kama ile iliyotokea poleni sana na naomba mzingatie maelekezo ya wataalamu” RC Mrindoko.
Lakini pia katika ziara hiyo akiwa katika mradi huo wa shule ameagiza ujenzi huo ukamilike mapema ili mwaka unapoanza wanafunzi waanze kupatiwa elimu katika shule hiyo, wakati huo amewataka wazazi kuhakikisha watoto wote walio katika umri wa kuanza masomo, wahakikishe waandikishwa ili kupata haki yao ya msingi.
RC Mrindoko katika ziara yake hiyo amewakumbusha wananchi wote Mkoa wa Katavi, kujitokeza kwa wingi tarehe 29 Oktoba ili kupiga kura ya kumchagua Rais, Wabunge na Madiwani, kwa kuzingatia utulivu na amani.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: