SERIKALI KUJENGA BARABARA YA NJIA NNE MKOANI MWANZA
Автор: Wizara ya Ujenzi
Загружено: 2025-08-05
Просмотров: 9304
Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS) imejipanga kikamilifu kuleta mapinduzi ya miundombinu katika Jiji la Mwanza kupitia ujenzi wa barabara ya njia nne kuanzia Mwanza Mjini hadi Usagara pamoja na njia ya mabasi ya mwendokasi, hatua inayolenga kufungua fursa mpya za kiuchumi kwa jiji hilo na mikoa jirani.
Akizungumza kuhusu mradi huo, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Ambrose Pascal amesema kuwa maandalizi ya ujenzi yamekamilika na utekelezaji utaanza mara tu baada ya kumpata Mkandarasi mshindi wa zabuni iliyotangazwa.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: