Nini kingetokea kama huyu mtu angeisikiliza sauti ya Mungu?
Автор: 7T7 MINISTRY
Загружено: 2022-12-16
Просмотров: 432
Inawezekana umeshikilia Kamba ya mahusiano yasiyo sahihi, na unashindwa kuachia hiyo Kamba kwa sababu unahisi ukiachia utaangukia kwenye mawe. Sauti ya Mungu ikisema achia, usisite kuachia, maana ni hakika kuwa Mungu amekuandalia mahusiano mengine bora zaidi yatakayokuokoa usiangukie kwenye mawe na kuvunjikavunjika.
Yawezekana umeshikilia biashara au kazi isiyo sahihi, na unaogopa kuachana nayo kwa sababu hujui utaishije. Sauti ya Mungu inasema achia hiyo Kamba maana yeye anajua namna ya kukuokoa usiangukie kwenye mawe.
Inawezekana umeshikilia Imani au dini isiyo sahihi kulingana na maandiko. Usiogope kuiacha hata kama inakupa maslahi fulani makubwa maana Mungu anajua namna ya kukuokoa usiangukie kwenye mawe na kuvunjikavunjika.
Biblia katika kitabu cha Yeremia 29 fungu la 11 inasema, “Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.”
Mwamini Mungu na kusikiliza sauti yake, maana yeye ndiye atakayekuokoa kutoka kwenye Kamba uliyoning’inia. Usipoiachia Kamba yako utakufa ukiwa bado unaning’inia hapo hapo. Kamba hiyo haikuokoi kamwe, ila itakufariji kwa muda mfupi na baadae itakuacha ufe mwenyewe.
Subscribe / @7t7ministryenglish24 ili upate kubarikiwa na Bible quizes za kiingereza
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: