Популярное

Музыка Кино и Анимация Автомобили Животные Спорт Путешествия Игры Юмор

Интересные видео

2025 Сериалы Трейлеры Новости Как сделать Видеоуроки Diy своими руками

Топ запросов

смотреть а4 schoolboy runaway турецкий сериал смотреть мультфильмы эдисон
dTub
Скачать

HALI YA MAISHA NGORONGORO MIEZI MIWILI BAADA YA MAANDAMANO NA UJUMBE WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

Автор: WATETEZI TV

Загружено: 2024-11-18

Просмотров: 2609

Описание:

Miezi miwili baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuagiza kurejeshwa kwa huduma za kijamii katika Tarafa ya Ngorongoro, matumaini mapya yameanza kuonekana, ingawa changamoto nyingi bado zinasalia. Ziara iliyofanywa mwezi Novemba 2024 na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) imethibitisha kuwa serikali imeanza kuchukua hatua za kurekebisha hali ya mambo, lakini kazi kubwa bado ipo mbele.

Taarifa iliyotolewa tarehe 18 Novemba 2024 na Mratibu Taifa wa THRDC Wakili Onesmo Olengurumwa, katika ziara hiyo, THRDC imebaini kuwa Serikali ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro imetenga bajeti ya shilingi bilioni mbili kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Miradi hii inajumuisha ukarabati wa shule, vituo vya afya, na miundombinu mingine muhimu ambayo imekuwa katika hali mbaya kwa miaka kadhaa. Mfano wa juhudi hizi ni shule ya msingi Ndian, ambayo imepangiwa Tsh milioni 111 kwa ukarabati wa madarasa nane, nyumba mbili za walimu, na vyoo. Vilevile, shule ya sekondari ya wasichana Ngorongoro itapokea Tsh milioni 108 kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wanafunzi na maabara ya kemia.

“Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wafugaji na Diwani wa Kata ya Alaileai, Mhe. Shutuk Kitamwas pia aliieleza kuwa baadhi ya miradi imeanza kutekelezwa, na miradi mingine imependekezwa kusubiri hadi mwishoni mwa mwaka kwa sababu za usalama, ikiwemo ukarabati wa shule. Viongozi wengine wakiwemo wenyeviti wa vijiji na madiwani waliofikiwa na ziara hii, nao wameonesha kutambua uwepo wa bajetit hii inayotengwa kwa ajili ya ukarabati wa maeneo ya huduma za kijamii”, imeeleza taarifa hiyo.

Upande wa demokrasia, kumeonekana kupiga hatua. Taarifa hiyo imeeleza kuwa Tarafa ya Ngorongoro inashika nafasi ya tatu kwa kuwa na idadi kubwa ya wapiga kura waliosajiliwa kwa uchaguzi wa 2024/2025.

“Hii inaonesha kuwa kuna wananchi wa Tanzania katika eneo hilo, na ni vyema kwao kutumia haki yao ya kidemokrasia. Pamoja na hayo, wana Ngorongoro sasa wanahisi kuwa na uhuru wao na uwepo wa viongozi wao wa serikali baada ya muda mrefu. Walieleza kuwa hata wanaona viongozi wakitembelea eneo hilo na kushughulikia shida zao, jambo ambalo ni faraja kubwa baada ya miaka michache iliyopita ambapo walionekana kama wahamiaji katika nchi yao”, imeeleza taarifa hiyo.

Pamoja na hatua hizi, bado kuna changamoto nyingi ambazo hazijatatuliwa. Huduma za afya za dharura, kama ndege ya Flying Medical Doctor, hazijarejeshwa, na ukosefu wa vibali kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za asili umesababisha baadhi ya wananchi kufikishwa mahakamani. Aidha, malalamiko ya wananchi kuhusu ada za wanafunzi wa Ngorongoro na uhaba wa bajeti kwa ajili ya elimu bado yanatolewa.

Wananchi wa Ngorongoro wanasisitiza umuhimu wa Rais Samia kutimiza ahadi yake ya kutembelea Tarafa hiyo ili kuwasikiliza moja kwa moja na kujadiliana kuhusu changamoto zinazowakabili. Ombi hili lilitolewa wakati wa maandamano ya amani ya Agosti 2024, ambapo wananchi walisisitiza umuhimu wa kushirikishwa zaidi katika maamuzi kuhusu mustakabali wa maisha yao.

Licha ya juhudi za serikali, THRDC inasisitiza kuwa ni muhimu kuharakisha utekelezaji wa mipango iliyopo na kuhakikisha kwamba haki za binadamu, huduma za kijamii, na juhudi za uhifadhi zinazingatiwa kwa usawa. Mtandao huo pia umetoa wito wa kushirikisha zaidi wadau wa maendeleo na watetezi wa haki za binadamu ili kuhakikisha kuwa changamoto za muda mrefu zinatatuliwa kwa ufanisi.

Wananchi wa Ngorongoro wanaendelea kuwa na matumaini huku wakiomba hatua zaidi zichukuliwe haraka ili kurejesha hali ya kawaida na kuhakikisha kwamba changamoto za kihistoria zinazowakabili zinapata suluhisho la kudumu.

HALI YA MAISHA NGORONGORO MIEZI MIWILI BAADA YA MAANDAMANO NA UJUMBE WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

Поделиться в:

Доступные форматы для скачивания:

Скачать видео mp4

  • Информация по загрузке:

Скачать аудио mp3

Похожие видео

🔴TAARIFA YA HABARI YA ASUBUHI.....DESEMBA 18,  2025

🔴TAARIFA YA HABARI YA ASUBUHI.....DESEMBA 18, 2025

DW Kiswahili Habari za Ulimwengu | Podcast | Dunia Yetu | Leo Mchana | 18.12.2025 | Swahili News

DW Kiswahili Habari za Ulimwengu | Podcast | Dunia Yetu | Leo Mchana | 18.12.2025 | Swahili News

THRDC YAFANYA ZIARA NGORONGORO YATOA MREJESHO UTEKELEZAJI AGIZO LA RAIS SAMIA

THRDC YAFANYA ZIARA NGORONGORO YATOA MREJESHO UTEKELEZAJI AGIZO LA RAIS SAMIA

KIJANA ANAYEIGIZA SAUTI YA RAIS SAMIA AWAVUNJA MBAVU MKUTANONI

KIJANA ANAYEIGIZA SAUTI YA RAIS SAMIA AWAVUNJA MBAVU MKUTANONI

MAHOJIANO YA MHE. RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI WA NCHINI TANZANIA.

MAHOJIANO YA MHE. RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI WA NCHINI TANZANIA.

🔴#Live:  RAIS SAMIA AONGELEA MKOPO wa KOREA ULIOZUA GUMZO MITANDAONI - ''KWA MIAKA 40''...

🔴#Live: RAIS SAMIA AONGELEA MKOPO wa KOREA ULIOZUA GUMZO MITANDAONI - ''KWA MIAKA 40''...

Film, który nie puści Cię aż do samego końca! | Ostatni ocalały | Filmy po polsku

Film, który nie puści Cię aż do samego końca! | Ostatni ocalały | Filmy po polsku

HOTUBA YA MHE. RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN WAKATI  WA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA JESHI LA POLISI.

HOTUBA YA MHE. RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN WAKATI WA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA JESHI LA POLISI.

Wanasheria Wajitosa Sakata la Ngorongoro, Mwabukusi Aelezea Hatua Zinazofuata.

Wanasheria Wajitosa Sakata la Ngorongoro, Mwabukusi Aelezea Hatua Zinazofuata.

🔴#Live: RAIS SAMIA AVUNJA UKIMYA MAUAJI ya MZEE ALI KIBAO - ATOA MSIMAMO KUHUSU MAANDAMANO...

🔴#Live: RAIS SAMIA AVUNJA UKIMYA MAUAJI ya MZEE ALI KIBAO - ATOA MSIMAMO KUHUSU MAANDAMANO...

RAIS SAMIA AKISHIRIKI KUAGA MWILI WA MBUNGE WA KIGAMBONI DKT. FAUSTINE NDUGULILE

RAIS SAMIA AKISHIRIKI KUAGA MWILI WA MBUNGE WA KIGAMBONI DKT. FAUSTINE NDUGULILE

MHE. RAIS DKT. SAMIA AKIWAAPISHA VIONGOZI WATEULE IKULU DAR ES SALAAM

MHE. RAIS DKT. SAMIA AKIWAAPISHA VIONGOZI WATEULE IKULU DAR ES SALAAM

THRDC: Tunapochelewa kufanya maridhiano ndivyo mambo yanavyozidi kuwa mengi

THRDC: Tunapochelewa kufanya maridhiano ndivyo mambo yanavyozidi kuwa mengi

Врач-Уролог предупреждает: Эта привычка УВЕЛИЧИВАЕТ простату!

Врач-Уролог предупреждает: Эта привычка УВЕЛИЧИВАЕТ простату!

WALIOCHOAMBIWA WANANCHI WA NGORONGORO RAIS SAMIA ATOA MSIMAMO HUU

WALIOCHOAMBIWA WANANCHI WA NGORONGORO RAIS SAMIA ATOA MSIMAMO HUU

DAKIKA 51 ZA MASWALI YA WAHARIRI WA HABARI KWA RAIS, AKITAJA MAKINIKIA

DAKIKA 51 ZA MASWALI YA WAHARIRI WA HABARI KWA RAIS, AKITAJA MAKINIKIA

🔴RAIS SAMIA AKISHIRIKI SHEREHE ZA KAMISHENI NA MAHAFALI KWA MAAFISA WANAFUNZI ARUSHA

🔴RAIS SAMIA AKISHIRIKI SHEREHE ZA KAMISHENI NA MAHAFALI KWA MAAFISA WANAFUNZI ARUSHA

MAKAMU MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NGORONGORO AHAMIA MSOMERA

MAKAMU MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NGORONGORO AHAMIA MSOMERA

Իսրայելցի զինվորականները գաղտնի գնացել են Բաքու

Իսրայելցի զինվորականները գաղտնի գնացել են Բաքու

RAIS SAMIA AKIPIGA KURA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

RAIS SAMIA AKIPIGA KURA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

© 2025 dtub. Все права защищены.

  • Контакты
  • О нас
  • Политика конфиденциальности

Контакты для правообладателей: [email protected]