Ufugaji Wa Samaki Kwa Mtaji Mdogo (Bustani ya Eden Ep 2)
Автор: AJE -FARMS ; MASHAMBA YANAYOTEMBEA
Загружено: 2025-10-03
Просмотров: 254
Hii video ni ya pili katika series za kukuonesha fursa ya kilimo biashara ukiwa una mtaji mdogo. Kwenye video hii tunasafisha BWAWA na kukagua ukuaji wa samaki waliopandwa kwenye BWAWA hili miezi 3 iliyopita.
Mradi huu ukikamilika tunatarajia uwe na uwezo wa kuzalisha TZS 100 - TZS 200 kila baada ya dakika 1 sawa na TZS 144,000 - 288,000 kwa siku na TZS 4,320,000 hadi TZS 8,640,000 kwa mwezi. Katika mradi huu tunayo mabwawa mawili ya samaki yaliyopandwa samaki aina ya kambale na sato. Mabwawa haya hutumika kufugia bata pia.
Mradi huu una miradi midogo zaidi ya 10 yote ikiwa ndani ya shamba la ekari 1 tu. Katika shamba hili hatutumii dawa au mbolea za VIWANDANI. Ni shamba linalofuata kanuni za KILIMO HAI (Organic Farming)
Shamba hili tulilizindua rasmi tangu mwezi Aprili mwaka huu (2025).
Fuatilia kila series ili kuelewa jinsi ya kuendesha kilimo kama biashara.
Itaendelea.... UJASIRI-wA-MALI
Aje Farmer
#ajefarms #mashambayanayotembea
#bustaniyaedenseries #ajefarms #viralvideo #farming #ufugaji #animals #kilimo #agriculture #cages #diet
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: