Mazishi ya kitaifa ya aliyekuwa Rais wa Msumbiji Samora Machel tarehe 28 Oktoba 1986.
Автор: Tulipotoka Zamani
Загружено: 2024-02-05
Просмотров: 1158
Usiku wa Tarehe 19 Oktoba mwaka 1986 Ndege iliyotengenezwa Urusi aina ya Tupolev TU 134A iliyombeba aliyekuwa Rais wa Msumbiji Samora Machel ilipokuwa ikitokea Zambia kurudi Msumbiji ilipoteza uelekeo na kwenda kudondoka katika vilima vya Lebombo karibu na mji mdogo wa Mbuzini nchini Afrika ya Kusini. Ajali hiyo ilisababisha kifo cha Rais huyo wa Msumbiji na watu wengine 34 waliokuwa ndani ya ndege hiyo. Ni watu 9 pekee ndio waliosalimika katika ajali hiyo akiwemo mlinzi wa Rais.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: