HARUSI YA IDI AMIN
Автор: Tulipotoka Zamani
Загружено: 2022-07-07
Просмотров: 667
Hii ilikuwa ni tarehe 1 Agosti 1975 ambapo aliyekuwa kiongozi wa Uganda, Idi Amin alimuoa Sarah, msichana ambaye alikuwa na umri wa miaka 19 tu wakati huo. Hiyo ilikuwa ni ndoa ya tano kwa Rais Amin. Sherehe za harusi hiyo zilihudhuriwa na viongozi wa nchi mbalimbali akiwemo Yasser Arafat aliyekuwa kiongozi wa kundi la ukombozi wa Palestina la PLO, Siad Barre aliyekuwa Rais wa Somalia, Jaafar El-Nimeiry aliyekuwa Rais wa Sudan, Daniel Arap Moi aliyekuwa Makamu wa Rais wa Kenya. Viongozi hao wote na wengine walikuwa Uganda kwa wakati huo wakihudhuria kikao cha Umoja wa nchi huru za Afrika (OAU) ambao Rais Amin alikuwa ndio Mwenyekiti wake kwa mwaka huo wa 1975.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: