NENO LA SIKU | Luka 9 | Maombi Ya Kushinda Roho Ya Kurudi Nyuma | Isaac Javan
Автор: Neno La Siku
Загружено: 2024-06-10
Просмотров: 4608
Leo tunasoma kitabu cha Luka sura ya tisa, na tunaenda kufanya maombi ya kushinda roho ya kurudi nyuma. Inawezekana umewahi kurudishwa nyuma kwenye maisha yako, mahali ambapo ulikuwa unaona unaenda vizuri, lakini ghafla kuna kitu kibaya kinatokea na mambo yanaharibika kwa namna ambayo inakulazimu uanze upya.
Katika ulimwengu wa roho ipo roho inayowakwamisha watu na kuwafanya warudi nyuma. Na lengo la hii roho ni kuwafanya watu wasitimize hatima zao walizowekewa na Mungu. Lakini Mungu ni mwaminifu, kwa sababu katika siku ya leo anaenda kukupigania na kukushindia. Nami nakuombea, kwamba baada ya maombi ya leo, ukaanze kupiga hatua na kusonga mbele kwenye maisha yako. Damu ya YESU inene mema kwa ajili yako. Amen!
Isaac Javan
+255 745 76 45 72
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: