SUA YAZINDUA MRADI WA KUBORESHA UZALISHAJI WA MAZAO KATAVI
Автор: BONGO PLAY TELEVISION
Загружено: 2025-12-18
Просмотров: 13
SUA YAZINDUA MRADI WA KUBORESHA UZALISHAJI WA MAZAO KATAVI
Katika juhudi za kupunguza umaskini wa kipato na kukabiliana na changamoto ya uzalishaji mdogo wa mazao ya kilimo, Chuo Kikuu cha Kilimo Cha Sokoine (SUA) kimeanza utekelezaji wa mradi mkubwa wa kuongeza tija ya kilimo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, mradi wenyw thamani ya zaidi ya shilingi milioni 400.
Mradi huo unalenga kuwainua wakulima wadogo ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakitegemea mbinu za kizamani za kilimo, hali iliyosababisha mavuno duni, uhaba wa chakula katika kaya, na kushuka kwa kipato cha familia nyingi katika wilaya hiyo.
Wakizungumza wakiwa katika mashamba ya wakulima wanaonufaika na mradi huo, wahadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo SUA, wamesema kuwa chanzo cha kuanzishwa kwa mradi huo ni hali ya uzalishaji mdogo wa mazao inayochangiwa kwa kiasi kikubwa na matumizi ya mbinu za jadi zisizoendana na mabadiliko ya teknolojia ya kilimo
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: