DC KOLIMBA AHIMIZA UTUNZAJI VYANZO VYA MAJI KWA HUDUMA BORA
Автор: Tangauwasa TV
Загружено: 2025-07-22
Просмотров: 72
Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini, Mhe. Dadi Kolimba amesisitiza juu ya umuhimu wa kuendeleza jitihada za uhifadhi na utunzaji wa vyanzo vya maji ili kufanikisha upatikanaji huduma ya uhakika kwa wananchi. Rai hiyo ameitoa wakati wa hafla ya mapokezi ya vifaa vitakavyotumika katika muendelezo wa utekelezaji wa mradi wa Kuboresha hali ya upatikanaji huduma ya maji Tanga awamu ya tatu (3) kupitia ufadhili wa Hatifungani ya Kijani.
"Tunajua kwa sasa upatikanaji huduma ya Maji katika Jiji la Tanga ni karibia asilimia 97, uboreshaji huu ukifanyika vizuri na unavyokusudia tutafikia silimia 100 na zaidi hivyo nitoe rai kuwa tuhakikishe tunasimamia yanzo vya maji ili mradi huu uweze kutekezeka kwa ufanisi"
Alisema DC Kolimba
Akizungumza pia wakati wa hafla hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga UWASA, Dkt. Fungo A. Fungo ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa mchango mkubwa katika kuwezesha utekelezaji wa mradi huu muhimu na kuainisha kuwa mradi umegawanyika katika sehemu kuu nne na vifaa hivi ambavyo vimepokelewa vitatumika katika sehemu ya mwisho ya mradi inayohusisha uendelezaji na ukarabati wa mabomba ili kufanikisha upatikanaji wa huduma bora na ya uhakika kwa wakazi wa maeneo yanayohudumiwa na Tanga UWASA.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: