Популярное

Музыка Кино и Анимация Автомобили Животные Спорт Путешествия Игры Юмор

Интересные видео

2025 Сериалы Трейлеры Новости Как сделать Видеоуроки Diy своими руками

Топ запросов

смотреть а4 schoolboy runaway турецкий сериал смотреть мультфильмы эдисон
dTub
Скачать

MUNGU ALITUUMBA ILI TUMJUE, TUMPENDE, TUMTUMIKIE, TUPATE KUFIKA KWAKE MBINGUNI.

Автор: Jifunze Katekesi (Katekisimu)

Загружено: 2022-04-23

Просмотров: 845

Описание:

MUNGU ALITUUMBA ILI…….
U hali gani mpendwa mfuatiliaji wa channel pendwa ya JIFUNZE KATEKESI, karibu tena katika mfululizo wa vipindi vyetu. Leo tunakuleteeni mada ihusuyo kusudio la Mwenyezi Mungu kutuumba yaani KWA NINI MUNGU ALITUUMBA? Tutaangalia makusudio manne ya Mungu kutuumba
Kanisa kupitia mafundisho ya katekesi, linatufundisha na ndivyo ilivyo, kuwa Mungu alituumba ili
• Tumjue
• Tumpende
• Tumtumikie
• Ili tupate kufika kwake mbinguni.
Kabla hatujaanza kutazama kusudio moja baada ya lingine, nikukumbushe usisahau ku”share na ku”subscribe” kwa kubonyeza alama ya kengele hapo chini.
Na sasa tuanze kupitia kusudio moja baada ya lingine. Kama tulivyoeleza hapo awali kuwa kusudio la kwanza kabisa ni kuwa Mungu alituumba ili tumjue. Sasa basi
1. Tunawezaje kumjua Mungu?
Kwanza kabisa, Mungu ni Roho halisi, na chochote kilicho cha kiroho katuwezi kukiona kwa macho yetu ya kibinadamu. Dokezo la kwanza linaloweza kutujuza juu uwepo wa Mungu, tunalipata kupitia vitu mbalimbali tunavyoviona. Kwa mfano, tukitazama milima, mito mikubwa, bahari, wanyama wakubwa, misitu mikubwa n.k. tunajiuliza chanzo cha haya yote ni nini? Au asili ya haya yote ni nani? Kwahiyo kupitia vitu tunavyoviona tunaweza kumjua Mungu kuwa ndiye asili na Muumba wa vitu hivyo.
Dokezo la pili linaloweza kutujuza juu ya uwepo wa Mungu, ni historia ya mwanadamu kupitia maandiko matakatifu. Biblia Takatifu, imeeleza vizuri mno juu ya uwepo wa Mungu kuanzia uumbaji, anguko la mwanadamu, matayarisho ya kumkomboa mwanadamu, ukombozi wa mwanadamu kwa njia ya mateso, kifo na ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristu. Haya yote yanatufanya tumjue Mungu.
Dokezo la tatu ni kuwa tunaweza kumjua Mungu kupitia mafundisho ya kanisa ambayo yanatolewa kupitia vipindi mbalimbali vya dini, pia kupitia maisha ya ushuhuda ya baadhi ya watu ambao wameonja uwepo wa Mungu kupitia hali fulani walizopitia katika maisha yao.
Na sasa tuhamie kwenye kusudio la pili la Mungu kutuumba sisi kwamba Mungu alituumba ili tumpende. Sasa basi….
2. Tunawezaje kumpemda Mungu?
Kwanza kabisa, tunaweza kumpenda Mungu kwa kuvipenda, kuvijali na kuvitunza viumbe alivyoviumba. Lakini pia kuzishika amri za Mungu, ni namna nyingine pia ya kumpenda Mungu. Amri za hizo ndizo hizi
• Usiabudu miungu mingine
• Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako
• Shika kitakatifu siku ya Mungu
• Waheshimu baba yako na mama yako
• Usiue
• Usizini
• Usiibe
• Usiseme uongo
• Usitamani mwanamke asiye mke wako
• Usitani mali ya mtu mwingine
Amri zote hizo kumi, zinadokeza kumpenda Mungu na Jirani.
Hivyo basi, Mungu alituumba ili tumpende kwa kuzishika Amri zake na kuwapenda jirani zetu bila kusahau kuvipenda viumbe vingine vilivyoumbwa naye kwani kulipenda boga lazima upende na ua lake.
Kusudio la tatu la Mungu kutuumba, ni kwamba ili tumtumikie. Sasa basi……
3. Tunawezaje Kumtumikia Mungu?
Tunaweza kumtumikia Mungu kadiri ya nafasi zetu zozote tulizonazo. Kumtumikia Mungu sio lazima uwe Padri au mtawa, bali katika wito wako wowote ulioitiwa, unaweza kumtumikia Mungu. Kwa maneno mengine, uwe mwalimu, mwanajeshi, bodaboda, rubani, mamant’ilie, mwanafunzi, raisi, muigizaji, muimbaji wa Bongo fleva nk. Unaweza kumtumikia Mungu katika nafasi yako uliyonayo.
Utume mkubwa ambao kila mbatizwa anao, ni kumpeleka Kristu kwa Watu. Kumtumikia Mungu kunadai Ushiriki kamili katika shughuli za kitume ambazo kanisa linafanya. Kwa mfano, kila mbatizwa ana wajibu wa kutoa zaka. Zaka hiyo inasaidia kumpeleka Kristu kwa watu, hivyo wewe bodaboda au mkulima, au muigizaji wa bongo movie n.k., fahamu kuwa unamtumikia Mungu kupitia nafasi uliyonayo kwa kusaidia shughuli za kitume.
Kusudio la mwisho la Mungu kutuumba ni kwamba….
4. ILI TUPATE KUFIKA KWAKE MBINGUNI
Mpendwa mfuatiliaji wa channel ya IJUE KATEKESI, kumjua Mungu, Kumpenda na Kumtumikia kunapaswa kuendane na kusudio la kufika kwake mbinguni. Chochote tufanyacho hapa duniani lazima kiwe na muono wa kutufikisha mbinguni; hilo ndilo Mungu anapenda sisi Watoto wake tuwe.
Mpendwa mfuatiliaji wa channel yetu ya IJUE KATEKESI, Mungu alituumba katika muungano wa Mwili na Roho, na kama nilivyoeleza hapo awali kuwa Mungu ni Roho halisi, hivyo hatuwezi kufika kwake isipokuwa tu mwili umetengena na roho kwa njia ya kifo. Hivyo hatupaswi kuogopa kifo kama kweli katika maisha yetu tumemjua Mungu, tumempenda na kumtumikia, maana kifo ni daraja la kutufikisha kwa Mungu tukiwa ndani ya Kristu Bwana wetu.
Kwa leo tuishie hapa, nizidi kukusihi usisahau ku“share”, ili usambaze upendo wa mafundisho haya kwa wengine na pia usisahau ku“subrcribe” ili kuwa wa kwanza kupata mafundisho endelevu kutoka channel hii pendwa ya JIFUNZE KATEKESI
Nikutakie siku Njema! Tumsifu Yesu Kristu!
#kanisakatoliki #kristo #katekeseimankatolik #mafundisho #jifunzekatekesi

MUNGU ALITUUMBA ILI TUMJUE, TUMPENDE, TUMTUMIKIE, TUPATE KUFIKA KWAKE MBINGUNI.

Поделиться в:

Доступные форматы для скачивания:

Скачать видео mp4

  • Информация по загрузке:

Скачать аудио mp3

Похожие видео

Три человека, которые тихо разрушают вашу жизнь после пятидесяти!

Три человека, которые тихо разрушают вашу жизнь после пятидесяти!

KWANINI TUNASALI SIKU YA JUMAPILI BADALA YA JUMAMOSI (SABATO)

KWANINI TUNASALI SIKU YA JUMAPILI BADALA YA JUMAMOSI (SABATO)

Как выучить 300 слов в день за 8 минут? Как учат слова разведчики и как советуют нейроученые!#mit

Как выучить 300 слов в день за 8 минут? Как учат слова разведчики и как советуют нейроученые!#mit

Mt. Kizito Makuburi - Maisha Yangu (Official Music Video)

Mt. Kizito Makuburi - Maisha Yangu (Official Music Video)

MUNGU ALIMUUMBA SHETANI ILI AMVUKUZE MBINGUNI AJE KUTUTESA WANADAMU?

MUNGU ALIMUUMBA SHETANI ILI AMVUKUZE MBINGUNI AJE KUTUTESA WANADAMU?

Нерассказанная история ДИНЫ — Тайна дочери ИАКОВА и сила восстановления

Нерассказанная история ДИНЫ — Тайна дочери ИАКОВА и сила восстановления

История Византии за 13 минут

История Византии за 13 минут

HII NI KWARESMA: JE, UMESAHAU NAMNA YA KUUNGAMA KWA PARDI? TAZAMA HII

HII NI KWARESMA: JE, UMESAHAU NAMNA YA KUUNGAMA KWA PARDI? TAZAMA HII

Bella Kombo ft. Evelyn Wanjiru & Neema Gospel Choir - Mungu Ni Mmoja (Official Video)

Bella Kombo ft. Evelyn Wanjiru & Neema Gospel Choir - Mungu Ni Mmoja (Official Video)

Jutarnja Molitva

Jutarnja Molitva

8 ЛОВУШЕК, которые люди преподносят тебе под видом ДОБРОТЫ! | Еврейская Мудрость

8 ЛОВУШЕК, которые люди преподносят тебе под видом ДОБРОТЫ! | Еврейская Мудрость

Лечебная СУСТАВНАЯ ГИМНАСТИКА! Утренняя зарядка!

Лечебная СУСТАВНАЯ ГИМНАСТИКА! Утренняя зарядка!

Joe Dassin Album Complet 2025 - The Best Of Joe Dassin 🏆 Joe Dassin Ses Plus Belles Chansons

Joe Dassin Album Complet 2025 - The Best Of Joe Dassin 🏆 Joe Dassin Ses Plus Belles Chansons

Nikupe Nini Mungu Wangu | B A Lukando | Sauti Tamu Melodies |Sadaka/Matoleo ~Skiza 7482438

Nikupe Nini Mungu Wangu | B A Lukando | Sauti Tamu Melodies |Sadaka/Matoleo ~Skiza 7482438

JAPO NI MACHUNGU OFFICIAL VIDEO - MAGENA MAIN MUSIC MINISTRY

JAPO NI MACHUNGU OFFICIAL VIDEO - MAGENA MAIN MUSIC MINISTRY

This Celtic Music Will Break Your Heart… And Heal Your Soul – Irish & Scottish Melodies

This Celtic Music Will Break Your Heart… And Heal Your Soul – Irish & Scottish Melodies

Понимание и анализ ферм

Понимание и анализ ферм

Утро с Богом: Отче Наш — Благодарность и Покров Божий | Утренняя Молитва

Утро с Богом: Отче Наш — Благодарность и Покров Божий | Утренняя Молитва

Почему средневековое железо никогда не ржавело, а ваше умирает через 2 года

Почему средневековое железо никогда не ржавело, а ваше умирает через 2 года

Самая красивая мелодия в мире...ВОССТАНОВЛЕНИЕ НЕРВНОЙ СИСТЕМЫ! Красивая мелодия, доводящая до слез

Самая красивая мелодия в мире...ВОССТАНОВЛЕНИЕ НЕРВНОЙ СИСТЕМЫ! Красивая мелодия, доводящая до слез

© 2025 dtub. Все права защищены.

  • Контакты
  • О нас
  • Политика конфиденциальности

Контакты для правообладателей: [email protected]